Mkuu wa wilaya ya Iringa Mh Richard
Kasesela amezindua mradi wa maji katika kijiji cha lupalama kilichopo katika
Tarafa ya kalenga Wilayani Iringa, Mradi huo umedhaminiwa na Shirika la E.P.I.C
(Everyday People Initiate Changes) la Marekani liloanzishwa na Mwanamuziki wa
Marekani Tinara Moore. Ambaye aliwahi kutembelea Tanzania na baadae kuamua kutoa
misaada mbalimbli.
Wanakijiji wa Lupalama kwa muda mrefu
wamekuwa wakitembea umbali mrefu kutafuta maji, “Tulikuwa tukilazimika kutembea
saa zima kufata maji mtoni nabado maji haya kuwa ya uhakika kwa maana kipindi
cha kiangazi mto ulikuwa una kauka jambo lililopelekea kupata shida kubwa sana
katika upatikanaji wa maji” anaeleza Bi
Theobadina Ngailo mkazi wa Lupalama anaongeza kuwa “Tulikuwa tunatumia hata
maji ya kwenye vidimbwi ambayo sio salama kwa matumizi ya binadamu kwani muda
mungine tulikuwa tukichangia maji hayo na mifugo jambo lilipolekea kulipuka kwa
magonjwa kama kuhara”.
Akizungumza wakati wa kukabidhi mradi huo
Muwakilishi wa E.P.I.C Tanzania Bwana Johnson Mkini Kisinda amsema kuwa mradi
huo umeghalimu pesa zaidi ya milioni therasini na tano hadi kukamilika “Hiki ni
kisima cha pili kwa urefu katika visima vyote tulivyo chimba kwani Lengo
lilikuwa kuchimba mita sabini tu ila tulikosa maji tukalazimika kuchimba mita
mia moja na themanini kwenda chini hadi kuyafikia maji”, pia ame waasa
wanakijiji wa Lupalama kuwa walinzi wa miundo mbinu hiyo ya maji kwani ni kwa
faida yao wenyewe.
Akikabidhi Mradi huo kwa wanakijiji wa
lupalama mkuu wa wilaya ya Iringa amewaomba
wana kijiji hao kuusimamia vema mradi huo kwani Ofisi yake ina mpango wa
kuhakikisha maji hayo yana sambazwa katika Maeneo Yote ya kijiji hicho ili
kuhakikisha upatikanaji wa maji kwa wingi “Ni ndoto yangu kuona Maji haya yana
wafikia wanakijiji wote wa lupalama ikibidi na maeneo ya Jirani wapate pia maji
haya nitoe agizo kwa serikali ya kijiji kuunda kamati ya kusimamia na kutunza
mradi huu ili uendelee kufanya kazi na kunufaisha wengi wakati mimi niki
hangaika kuona jinsi gani tunapata pampu ya Umeme ikishindikana hata ya kutumia
nguvu ya jua ili tusambaze maji haya sehemu nyingi zaidi”.
Pia ameagiza Serikali ya kijiji Kuanza
mara moja Mchakato wa ujenzi wa kituo cha afya kijijini hapo kwani ni kero ya
muda mrefu hasa kwa akina mama kwani wana lazimika kutembea kilomita saba kufuata
huduma ya afya “Nawaombeni Zoezi hili lianze mapema sana na ikibidi kila mwanakijiji
ashiriki kukusanya mawe ya ujenzi na pindi mkiwa tayali ujenzi uanze mara moja”.
Katika hotuba yake Mkuu wa wilaya pia amehimiza
watu kutunza chakula “ mvua mwaka huu sio za kuridhisha hivyo basi ipo hofu ya
kukosekana chakula ni muhimu wananchi wakatunza chakula na kulima mazao yenye
kuhimili ukame”
Post a Comment