Mkuu wa wilaya ya Iringa Mh Richard
Kasesela amepiga Marufuku ukataji wa miti katika wilaya ya Iringa, akizungumza
katika mkutano ulio wakutanisha wadau mbali mbali wa mazingira ulioandaliwa na
asasi isiyo ya kiserikali ijulikanayo kama LEAT lengo likiwa ni kuiwezesha jamii na Serikali
kushiriki , kujadili na kufanya maamuzi ya pamoja katika usimamizi wa maliasili
kupitia mfumo wa ufuatiliaji wa uwajibikaji (UJU).
“Ni
marufuku kukata miti katika wilaya yangu na nitoe agizo kwamba hata ukiwa na
kibali hakikisha unapata na barua toka katika ofisi ya mkuu wa wilaya kinyume
na hapo utakuwa umekiuka taratibu tulizo jiwekea” Amesema Mh kasesela, “ukataji
wa miti umekuwa na madhara makubwa sana kwa mfano angalieni Kijiji Mfyome palivyo
hivi sasa ni tofauti kabisa na palivyo kuwa miaka ya nyuma ilikuwa nadra sana
kuona ardhi ukiwa juu katika eneo lile lakini angalia hivi sasa jinsi palivyo
haribika hii yote ni kwakuwa miti inakatwa hovyo”
aliendelea
Mkuu wa wilaya.
Katika
hotuba yake ameweka wazi pia mkakati wa Serikali kuhamisha wote waliojenga
katika vyanzo vya maji pia wanao fanya shughuli zozote ambazo si rafiki na
vyanzo hivo ikiwemo kufyatua tofari na kulima (Vinyungu) wataondolewa .“Hivi
sasa tumeanza zoezi la kukamata tofari zote zilizo katika vyanzo vya maji na
hadi sasa tumesha kamata tofari zisizo pungua laki moja na zote zitaenda
kujenga madarasa” amesisitiza pia kuwa ni marufuku kufanya shughuli yeyote mita
sitini toka kilipo chanzo cha maji na atakae kiuka agizo hilo taratibu za
kisheria zitafata mkondo wake.
Mh
Kasesela amependekeza kuwa uanzishwe ufugaji nyuki katika maeneo ambayo
hayatumiki “Nadhani katika baadhi ya maeneo tunaweza fanya ufugaji wa nyuki
kwanza watakuwa walinzi wa misitu yetu pili watakuwa chanzo cha kipato pia
ningependekeza wale nyuki wakubwa” , mkutano huo uliowakutanisha madiwani na
wadau toka MBOMIPA , NJUMIKIK na wawakilishi toka Pawaga ,Idodi , Tungamalenga
, Iringa mjini , Karenga na maeneo mengine ya Wilaya ya Iringa.
Akimkaribisha
Mwenyekiti wa Jumuiya ya utunazaji Maliasili Bwana Ngola Magosi amesema “ kumekuwa na
changamoto kubwa katika utunzaji wa mali asili , vijiji havitoi kipaumbele
suala la misitu, viongozi na watendaji kujiusisha na uvunaji haramu wa misitu,
ushirikiano mdogo uliopo kati ya jeshi la polisi na suala zima la kusimamia
misitu. Haya yote yanafanya kazi iwe ngumu sana”
Mkutano
huo ulijumuisha madiwani, wakuu wa idara wa halmshauri ya Iringa, watendeaji
pamoja na jumuia za watunza maliasili. Mkutano umeazimia kuitisha kikao cha
viongozi wa ngazi za juu akiwemo Mkuu wa mkoa, wakuu wa wilaya wote,
wakurugenzi wa halmashauri pamoja na wenyeviti wa halmashauri Pia mashirika
yasiyo ya kiserikali yanayo husika na mali asili.
Angalia Video hapa Chini.....
Post a Comment